• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais mpya wa Malawi aapishwa na kutoa wito kwa umoja

    (GMT+08:00) 2019-05-29 09:58:03

    Rais mpya wa Malawi Peter Mutharika ameapishwa kwa muhula wake wa pili ambao pia ni wa mwisho, huku akitoa wito kwa taifa kushikamana ili kutimiza matarajio ya nchi hiyo.

    Bw. Mutharika amewataka washindani wake kukubali ushindi wake kwa sababu kutakuwa na mshindi mmoja tu, huku akiwashukuru wananchi wa Malawi kwa kumpigia kura na kuongeza kuwa ushindi wake ni wa watu, utawala wa sheria na demokrasia.

    Bw. Mutharika alishinda uchaguzi kwa kupata asilimia 38.57 ya kura zote, huku mshindani wake mkuu Bw. Lazarus Chakwera kutoka kundi kuu la upinzani MCP akipata asilimia 35.41 ya kura zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako