• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Michuano ya tenisi ya wazi ya Ufaransa- Petra Kvitova ajitoa, Federer arejea kwa kishindo

    (GMT+08:00) 2019-05-29 10:38:51

    Bingwa mara mbili wa michuano ya tenesi ya Wimbledon, Petra Kvitova amejiondoa katika raundi ya kwanza ya michuano ya wazi ya Ufaransa kutokana na majeraha ya mkono.

    Kvitova raia wa Jamhuri ya Czech na anayeshikilia nafasi ya 6 kwa ubora wa mchezo huo duniani, alikuwa acheze na Sorana Cirstea raia wa Romania.

    Mchezaji huyo pia ametangaza kuwa hatashiriki michuano ya wazi ya Italia inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi huu mjini Rome ambapo alitarajiwa kucheza na Maria Sakkari raia wa Ugiriki.

    kwa upande wa wanaume, mchezaji Roger Federer amefanikiwa kutinga mzunguko wa pili baada ya kumfunga Lorenzo Sonego kwa seti tatu mfululizo.

    Federer ambaye ana mataji 20 kibindoni, alishinda kwa seti 6-2, 6-4 na 6-4

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako