• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Newcastle United yauzwa kwa Bilionea wa Kiarabu, ni mpwa wa mmiliki wa Manchester City, Sheikh Mansour

    (GMT+08:00) 2019-05-29 10:39:06

    Mmiliki wa klabu ya Newcastle United, Mike Ashley ameripotiwa kufikia makubaliano ya kuiuza timu hiyo kwa mpwa wa mmiliki wa Manchester City, Sheikh Mansour kwa dau la pauni milioni 350.

    Gazeti la The Sun limeripoti kuwa, mmiliki huyo mpya anayejulikana kwa jina la Khaled bin Zayed Al Nehayan ni miongoni mwa wanafamilia ya kifalme kutoka Abu Dhabi ambapo mwaka jana alishindwa kuinunua Liverpool baada ya kutakiwa kutoa dau la pauni bilioni mbili.

    Taarifa zinaeleza kuwa tayari mkataba baina ya Ashley na Khaled umeshasainiwa tayari kuichukua klabu hiyo kwa pauni milioni 350 na tayari umeshafikishwa kwa wanaohusika na ligi kuu. Mpaka sasa klabu ya Newcastle haijatoa taarifa rasmi

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako