• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirikisho la Uchumi wa Ulaya na Asia lajitahidi kupanua ushirikiano na nchi mbalimbali

  (GMT+08:00) 2019-05-29 18:09:03

  Waziri mkuu wa Russia Bw. Dimitri Medvedev amesema Shirikisho la Uchumi wa Ulaya na Asia limejitahidi kupanua ushirikiano na nchi mbalimbali, ambapo linatarajia kusaini makubaliano ya biashara huria na nchi kadhaa.

  Bw. Medvedev amesema, shirikisho hilo linatarajia kusaini makubaliano hayo na Singapore, Israel na India kwa haraka, na pia linaendelea kushauriana na nchi nyingine.

  Habari zinasema, mwezi wa Mei mwaka jana shirikisho hilo lilisaini makubaliano na Iran kujenga eneo la biashara huria, ambalo mpango wake kamili utamalizika ndani ya miaka mitatu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako