• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Waziri aingilia kati kiwanda cha kahawa.

    (GMT+08:00) 2019-05-29 19:17:41

    Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda, ameitaka Tume ya Ushirika nchini kukitazama kiwanda cha kukoboa kahawa cha Tanganyika Coffee Curing Company (TCCCo) Ltd, kilicho manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro kwa jicho la ziada ili kuongeza uzalishaji. Alitoa agizo hilo jana alipotembelea kiwanda hicho na kuahidi kuitisha kikao kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Moshi kwa lengo la kuangalia namna ya kukabiliana na changamoto zinazokikumba kiwanda hicho. Alisema tume hiyo ina jukumu kubwa la kuhakikisha uzalishaji unaongezeka kwa kuwa kilikuwa na uwezo wa kukoboa tani 50,000 kwa mwaka, lakini sasa kinakoboa tani chini ya 1,000 kwa mwaka.

    Kakunda pia aliomba mahakama kutenda haki kwa watu wote ambao wamehujumu zaidi ya shilingi bilioni 1.2 zilizotengwa kwa ajili ya kununulia mitambo na serikali imeshawafikisha katika mikono ya sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako