• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya wageni 1,300 kutoka Afrika wathibitisha kushiriki kwenye maonesho ya kwanza ya biashara kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2019-05-29 20:05:45

    Hadi kufikia tarehe 24 Mei, wageni na wafanyabiashara zaidi ya 1,388 kutoka nchi 52 za Afrika walikuwa wamejiandikisha kuhudhuria maonesho ya kwanza ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika, yatakayofanyika tarehe 27 hadi 29 mwezi ujao mjini Changsha, mkoani Hunan.

    Maonesha hayo hadi sasa yamevutia jumla ya miradi 233 ya ushirikiano yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 74.7. Kutakuwa na maeneo sita yenye eneo la meta elfu 43 za mraba, zikiwa na mabanda ya taifa na maeneo ya kuonesha mafanikio ya makampuni na fursa ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi za Afrika.

    Pia kutakuwa na maonesho kwenye mtandao na ukumbi wa maonesho utakaoanzishwa kwa muda mrefu kwa ajili ya kuonesha bidhaa za Afrika zenye ubora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako