• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya fedha ya Marekani yasema hakuna mshirika mkubwa wa biashara anayefanyia ujanja sarafu yake

    (GMT+08:00) 2019-05-29 20:14:27

    Wizara ya fedha ya Marekani imesema hakuna mshirika wake mkubwa wa biashara anayeweza kutajwa kuwa anafanyia ujanja sarafu yake.

    Kwenye ripoti yake ya nusu mwaka kuhusu sera za kimataifa za uchumi na viwango vya ubadilishaji wa fedha, iliyoitoa kwenye bunge la Marekani, wizara hiyo imesema hakuna mshirika mkubwa wa biashara anayefikia vigezo vinavyoweza kutajwa kuwa anafanyia ujanja sarafu yake, kwenye kipindi cha robo nne za mwaka ulioishia Desemba 2018.

    Hata hivyo wizara hiyo imeziweka China, Ujerumani, Ireland, Italia, Japan, Korea Kusini, Malaysia, Singapore na Vietnam kwenye "orodha ya nchi zinazofuatiliwa" ikiwa na maana sera za ubadilishaji fedha za nchi hizi zinafuatiliwa kwa makini na serikali ya Marekani.

    Ripoti hiyo imepitia sera za nchi 21, ambazo thamani yake ya biashara na Marekani ni zaidi ya dola bilioni 40 za kimarekani kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako