• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wazitaka nchi za nje kutoingilia kati mambo ya Sudan

    (GMT+08:00) 2019-05-30 08:39:09

    Umoja wa Afrika umehimiza haja kwa utatuzi wa ndani wa haraka wa mgogoro wa hivi sasa nchini Sudan juu ya msingi wa kuheshimu nia na matumaini ya watu wa nchi hiyo.

    Baraza la Amani na Usalama la Umoja huo (PSC) limetoa taarifa likitaka nchi za nje kuacha uingiliaji ambao unaweza kufanya hali ya kisiasa nchini Sudan kuwa mbaya zaidi.

    Taarifa hiyo pia imesisitiza tena matumaini halali ya watu wa Sudan kwa nafasi wazi za kisiasa, ili kuwezesha demokrasia na kuchagua idara zinazoweza kuwawakilisha na kuheshimu uhuru na haki za binadamu.

    Baraza hilo pia limezitaka pande husika za Sudan kulinda maslahi ya taifa lao juu ya mambo yote mengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako