• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mchango wa vifaa vya tiba katika hospitali nchini Rwanda

    (GMT+08:00) 2019-05-30 09:05:45

    Kikosi cha 19 cha matibabu cha China nchini Rwanda kimekabidhi msaada wa vifaa vya tiba kwenye hospitali ya Masaka iliyoko mji mkuu Kigali.

    Msaada huo uliotolewa na serikali ya China, unaendana na mahitaji ya hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na mashine za vipimo kwa ajili ya idara ya magonjwa ya tumbo.

    Mkurugenzi wa hospitali ya Masaka Marcel Uwizeye ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, msaada huo ni muhimu sana kwa hospitali hiyo na kwa watu wa huko. Amesema vifaa vya tiba vitatumika kwa ajili ya matibabu ya Wanyarwanda na pia kwa ajili ya elimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako