• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Uwanja wa Wanda wanogesha fainali ya Liverpool na Spurs

    (GMT+08:00) 2019-05-30 09:06:02

    Wakati wadau wa soka wakisubiri usiku wa mabingwa utakaokutanisha mafahali wawili kutoka kwa Malkia Elizabeth, Majogoo wa jiji Liverpool na watoto wa mjini Tottenham Hotspurs, huko mitaani mashabiki wameanza kutambiana kuhusu mechi hiyo na uwanja wa Wanda Metropolitano.

    Jumamosi Juni mosi macho na masikio yataelekezwa jiji la Madrid, kwenye uwanja wa Wanda unaoruhusu mashabiki 67,829 kushuhudia dakika 90 za mtanange huo wa vijana wa Mauricio Pochettino dhidi ya vijana wa Jurgen Klopp.

    Mechi itakuwa ngumu kutokana na Liverpool kucheza kwa mara ya pili mfululizo michuano hiyo huku Tottenham wao ni fainali yao ya kwanza tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo miaka 136 iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako