• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Straika wa Rwanda asaini Yanga miaka miwili

    (GMT+08:00) 2019-05-30 09:06:46

    Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Issa Bigirimana amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya Yanga ya Tanzania akitokea klabu ya APR ya Rwanda.

    Usajili huo umefanyika kutokana na pendekezo la kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye amepewa majukumu yote hivi sasa ya kuchagua wachezaji.

    Huyu anakuwa mchezaji wa pili wa Yanga baada ya kumalizana na Tshishimbi wa DRC aliyeongeza pia miaka miwili. Usajili umeendelea kushika kasi hivi sasa ikiwa ni baada ya ligi kumalizika juzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako