• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Mbio za Diamond League, wanariadha kuonyeshana ubabe

    (GMT+08:00) 2019-05-30 09:07:09

    Bingwa wa mbio za mita 1,500 wa Diamond league za mwaka 2018 Timothy Cheruiyot wa Kenya amesema anamatumaini ya kushinda mbio hizo za duru ya tatu zitakazofanyika leo jijini Stockholm Sweden.

    Katika mashindano yaliyofanyika mwezi huu mjini Doha, Qatar Cheruiyot aliambuliwa nafasi ya pili, hivyo sasa anataka kutorudia makosa na kuhakikisha anashinda mbio hizo.

    Cheruiyot anakabiliwa na ushindani mkali toka kwa wanariadha watatu wa Norway na wawili kutoka Ethiopia.

    Kwa upande wa wanawake, malkia wa dunia wa mbio za mita 5,000 Hellen Obiri anatarajiwa kuendeleza ubabe wake dhidi ya wakenya wenzake na waethiopia. Kukosekana kwa Caster Semenya wa Afrika Kusini, Francine Niyonsaba wa Burundi katika mbio za mita 800, kutawaacha washindani wengine wakipata ahueni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako