• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yaihimiza Tume ya Umoja wa Mataifa iunge mkono mipango ya maendeleo ya nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2019-05-30 09:09:36

    Sudan Kusini jana imeihimiza Tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo (UNMISS) iunge mkono mipango ya maendeleo licha ya operesheni za kulinda amani, kwani nchi hiyo changa inafufuka kutoka mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka mitano.

    Naibu waziri wa ulinzi wa Sudan Kusini Bw. Malek Ruben Riak amesema, UNMISS inapaswa kuunga mkono shughuli za maendeleo, ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu ya afya, elimu na barabara, na kutoa mafunzo kwa maofisa wa serikali ili kujenga uwezo wao.

    Vilevile amesifu mchango wa askari wa kulinda amani kutoka China, Uingereza, Japan, Bangladeshi, Rwanda na Korea Kusini kwa kuchangia ujenzi wa miundombinu nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako