• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Nigeria aapishwa kwa muhula wa pili

    (GMT+08:00) 2019-05-30 09:20:06

    Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ameapishwa kwa muhula wa pili wa miaka minne.

    Rais Buhari na makamu wake Yemi Osinbajo walikula kiapo jana Jumatano kwenye uwanja wa Eagle ulioko katikati ya mji mkuu, Abuja.

    Kaimu mwanasheria mkuu wa Nigeria Tanko Muhammad alisimamia kiapo cha rais, kikifuatiwa na kushushwa na kupandishwa kwa bendera ya taifa na ya ulinzi, na kupigwa mizinga ya heshima mara 21.

    Hakuna viongozi wa nchi za nje waliohudhuria halfa hiyo. Wageni waliohudhuria ni pamoja na viongozi wa usalama, mabalozi, na viongozi wa mahakama na wafanyabiashara wakubwa.

    Buhari aliapishwa kwa mara ya kwanza kuwa rais wa Nigeria Mei 29 mwaka 2015, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo kwa mgombea wa upinzani kuchukua madaraka kutoka kwa rais aliyekuwepo madarakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako