• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapata mkopo wa dola za kimarekani milioni 750 kutoka Benki ya Dunia

    (GMT+08:00) 2019-05-30 09:20:27

    Benki ya Dunia imesema imeidhinisha mkopo wa dola za kimarekani milioni 750 kwa Kenya ili kuunga mkono mageuzi ya nchi hiyo katika nyanja za kilimo, nyumba, teknolojia ya kidijitali na usimamizi wa kifedha.

    Mkopo huo utaiunga mkono Kenya kuendeleza mageuzi yake ili kuimarisha ukuaji shirikishi, kuharakisha juhudi za kupunguza umaskini na kutimiza Ruwaza yake ya Mwaka 2030 ya kuwa nchi ya viwanda yenye kipato cha kati.

    Mkurugenzi ya tawi la Benki ya Dunia nchini Kenya Bw. Felipe Jaramillo amesema, mkopo huo unatarajiwa kuwanufaisha wakenya wa kawaida kupitia kuhakikisha ruzuku za kilimo zinawafikia wakulima wenye kipato cha chini, kuwashitaki wale waliojihusisha na vitendo vya ulaghai, kuongeza upatikanaji wa nyumba za bei nafuu, na kuboresha uwezo kukusanya mapato.

    Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Kenya imekuwa moja ya nchi za Afrika kusini mwa Sahara zilizokua kwa kiasi kiuchumi katika mwongo uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako