• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msumbiji kufanya mkutano wa wafadhili kwa ajili ya ukarabati baada ya janga la kimbunga

    (GMT+08:00) 2019-05-30 09:20:45

    Ofisi ya Ukarabati Baada ya Janga la Kimbunga nchini Msumbiji imesema huko Beira kuwa, zaidi ya washirki 700 wamethibitisha kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa wafadhili utakaofanyika mjini humo kuanzia kesho.

    Mkurugenzi wa ofisi hiyo Bw. Francisco Pereira ameeleza imani yake kuwa mkutano huo utaisaidia serikali kukusanya fedha zinazohitajika zaidi ya dola bilioni 3 za kimarekani kwa ajili ya nchi hiyo kurudisha uchumi na jamii yake katika hali ya kawaida baada ya kukumbwa na kibunga Idai na Kenneth.

    Ofisa huyo amesema ukarabati wa miundombinu utatumia kiasi kikubwa cha fedha hizo, ikifuatiwa na ujenzi wa nyumba.

    Zaidi ya watu 640 walifariki na wengine milioni 1.85 waliathiriwa na vibunga hivyo vya Idai na Kenneth.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako