• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yampongeza Mutharika kuchaguliwa tena kuwa rais wa Malawi

  (GMT+08:00) 2019-05-30 09:37:21

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, China inampongeza Bw. Peter Mutharika kuchaguliwa tena kuwa rais wa Malawi, na kuamini kuwa chini ya uongozi wake, Malawi itapata maendeleo makubwa zaidi.

  Tume ya uchaguzi ya Malawi imetangaza matokeo ya uchaguzi mkuu yakionesha kuwa rais wa sasa ambaye pia ni kiongozi wa chama cha DPP Bw. Mutharika ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 38.57 ya kura zote na kuanza muhula mpya wa miaka mitano.

  Bw. Lu amesema, China inatilia mkazo katika kuendeleza uhusiano na Malawi, na kupenda kufanya juhudi pamoja na nchi hiyo kuimarisha kwa pande zote mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili na kunufaisha nchi hizo mbili na watu wao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako