• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwekezaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika nchini Morocco wazidi dola za kimarekani bilioni 1.4

    (GMT+08:00) 2019-05-30 09:40:42

    Ofisi ya waziri mkuu wa Morocco imesema, uwekezaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB nchini humo umezidi bilioni 1.4 za kimarekani, ambao unahusisha sekta za maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii.

    Taarifa hiyo imekuja baada ya mazungumzo kati ya waziri mkuu wa Morocco Saad Eddine El Othmani na makamu wa rais wa AfDB anayeshughulikia maendeleo ya kikanda, ushirikiano na biashara Bw. Khaled Sherif.

    Kwenye mazungumzo hayo, pande hizo mbili zimejadili njia ya kuimarisha na kupanua uhusiano wa kiwenzi kati yao, pia zimezungumzia kukuza ajira, kuongeza thamani ya viwanda kwenye pato la ndani GDP, kuimarisha ushindani wa uchumi wa Morocco, kuinua nafasi zake katika vigezo vya kimataifa, na kuongeza mvuto wake kwa uwekezaji wa kigeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako