• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa Kamati ya biashara kati ya Marekani na China aonya kuwa ni hatari kwa kutatua masuala ya uchumi na biashara kwa njia ya ushuru

    (GMT+08:00) 2019-05-30 10:29:03

    Mkuu wa Kamati ya biashara kati ya Marekani na China Bw. Craig Allen amesema, Marekani haipaswi kuchukua sera ya ushuru wa forodha kuwa mbinu ya kutatua masuala ya kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili.

    Amesema anatumaini kuwa China na Marekani zitafikia mapema makubaliano ya biashara kwa mazungumzo yenye uwazi na kuheshimiana, ili kuweka mazingira yenye utulivu kwa ajili ya mawasiliano ya uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili.

    Bw. Allen amesema hayo alipohudhuria Mkutano wa 5 wa Baraza la wakuu wa mikoa na magavana wa majimbo kati ya China na Marekani uliofanyika hivi karibuni. Pia ameeleza kuwa mazungumzo yanatakiwa kutatua matatizo, na siyo kuchochea mvutano, na kwamba ikiwa pande hizo mbili zitaweza kufikia mapema makubaliano ya kibiashara, si kama tu zitatatua kwa ufanisi mgogoro wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, vilevile itanufaisha sekta mbalimbali zinazohusiana na uhusiano kati ya pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako