• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Serikali ya Tanzania yatenga bilioni 53.5 kukopesha vijana, wanawake na walemavu

    (GMT+08:00) 2019-05-30 18:47:42

    Serikali ya Tanzania imetenga Sh53.5 bilioni kwa ajili ya kukopesha vijana, wanawake na walemavu katika bajeti ya mwaka 2019/2020 ambazo halmashauri zote nchini zitatakiwa kuzitoa kwa mujibu wa sheria.

    Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo amesema fedha hizo zinatolewa kama mkopo kwa makundi hayo kupitia Halmashauri zote nchini na akawaagiza wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanatoa fedha hizo.

    Pia Jafo amesema mwaka jana Serikali iliagiza kila mkoa kujenga viwanda ambapo walikusudia kuanzisha viwanda zaidi ya 2500 lakini utekelezaji wake umevuka lengo na kufikia viwanda zaidi ya 4,000 vilivyoanzishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako