• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya yapokea mkopo wa dola milioni 750 kutoka benki ya dunia

    (GMT+08:00) 2019-05-30 18:53:55

    Benki ya dunia imeidhinisha mkopo wa dola milioni 750 kwa Kenya kufuatia ombi lililotolewa na serikali.

    Jumatano benki hiyo imesema kuwa mkopo huo utafadhili shughuli za mageuzi muhimu, kuhimiza uwazi, ushindani na kupunguza ufisadi kwenye sekta ya kilimo.

    Mkopo huo pia kwa mujibu wa benki ya dunia utasaidia uendelezaji wa mpango wa serikali wa dijitali kama vile utoaji wa vitambulizho vipya na kusaidia kufikisha huduma za intaneti kwa wakenya wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako