• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Tanzania mbioni kukabili changamoto za uwekezaji

    (GMT+08:00) 2019-05-30 18:56:37

    Waziri wa Uwekezaji) nchini Tanzania Angellah Kairuki amewaeleza wawekezaji kutoka Uingereza kuwa miezi sita ijayo changamoto za uwekezaji nchini Tanzania zitakuwa historia.

    Kairuki ameeleza katika mkutano kati ya Serikali na wawekezaji hao uliofanyika jijini Dar es Salaam.

    Amesema changamoto zote zitapata ufumbuzi kwa maelezo kuwa hivi karibuni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alifanya mkutano na mawaziri wote na kuwapa maelekezo kuhusu mwongozo wa kuboresha mazingira ya biashara na kuwataka wahakikishe kila wizara haiwi kikwazo katika uwekezaji.

    Amesema anatarajiwa kuwa hatua ambazo Serikali inachukua Uingereza itaendelea kuwekeza zaidi kwa kuzingatia mpango wa nchi hiyo wa kuongeza uwekezaji Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako