• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapunguza kwa nusu idadi ya watoto waliodumaa kwa muda wa miaka 20

    (GMT+08:00) 2019-05-30 19:05:25

    China imepunguza idadi ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wanaodumaa kutokana na lishe duni kwa asilimia 54, katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

    Kwenye ripoti iliyotolewa na Shirika la Save the Children siku moja kabla ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya watoto ambayo ni Juni Mosi, imefahamika kuwa alama za China zimeongezeka kwa 80 kutoka 861 hadi 941, kutokana na kupungua kwa idadi ya vifo vya watoto na utapiamlo.

    Ripoti hiyo imelinganisha takwimu za mwaka 2000 na mwaka 2018, kwa kuangalia viashiria nane vya utoto mzuri, vifo kabla ya wakati, kudumaa, elimu, utumikishaji wa watoto, ndoa za utotoni, uja uzito wa utotoni, mauaji ya watoto na kutokuwa na makazi.

    Ripoti hiyo inasema zaidi ya nusu ya watoto waliondokana na kudumaa wako barani Asia, na nusu yao wako China na India.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako