• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yalaani Marekani kwa kuiwekea Huawei vikwazo bila ya shahidi

    (GMT+08:00) 2019-05-30 19:05:38

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo amesema, hivi karibuni Marekani imekuwa ikifanya juhudi chini juu kuwashawishi wamarekani na watu wa nchi nyingine waamini kuwa kampuni ya Huawei inaleta matatizo ya kiusalama, lakini kichofuatiliwa ni kama Marekani ina shahidi au la.

    Bw. Lu Kang amesema hayo kutokana na habari zinazosema, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo hivi karibuni amesema, ushirikiano kati ya makampuni na serikali ya Marekani unafuata sheria ya Marekani, lakini hali ni tofauti nchini China. Amesema kampuni ya Huawei ni mbinu ya serikali ya China, na zina uhusiano wa karibu. Vilevile msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema Marekani ina shahidi za kutoa mswada wa kuweka vizuizi kwa mashirika ya kiserikali ya Marekani kutumia vifaa vya Huawei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako