• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kauli za Marekani kuhusu kufikia makubaliano na China zina utata.

    (GMT+08:00) 2019-05-30 19:14:53

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng leo hapa Beijing amesema habari zinazotolewa na Marekani hivi karibuni ni tofauti, kuna wakati inatangaza kuwa huenda itafikia makubaliano na China mara moja, lakini wakati mwingine inatangaza kuwa haijamaliza maandalizi ya kufikia makubaliano na China, na hali hii inaifanya China iwe na mashaka kuhusu udhati wa Marekani.

    Bw. Gao Feng amesema Marekani imechochea mvutano wa kibiashara, na kufanya vitendo vya makosa katika sekta nyingine, na kuvunja msingi na mazingira ya kufanya mazungumzo, kwa hiyo inapaswa kuwajibika na makosa hayo. Amesema China siku zote inaona ushirikiano ni chaguo pekee na sahihi kwa China na Marekani.

    Pia amesisitiza kuwa ushirikiano una kanuni, na majadiliano yana mstari wa mwisho, na China haitarudi nyuma katika masuala makubwa ya kimsingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako