• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bibi Peng Liyuan akutana na wanafunzi wa kimataifa wa shahada ya pili wa Chuo cha Wanawake cha China

    (GMT+08:00) 2019-05-30 19:35:39

    Mke wa rais wa China Bibi Peng Liyuan leo hapa Beijing amekutana na wanafunzi wa kimataifa wa shahada ya pili wa Chuo cha Wanawake wa China. Amesema anatumai wanafunzi hao wakirudi nyumbani wataendelea kuwa daraja la kuunganisha China na nchi zao, ili kutoa mchango wao kwa ajili ya mambo ya wanawake wa dunia nzima na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya binadamu.

    Bibi Peng Liyuan amesema, China inafuatilia sana mambo ya wanawake, na inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali katika sekta za wanawake.

    Katika mkutano wa kilele wa wanawake wa dunia wa mwaka 2015, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuwaalika wanawake elfu 30 kutoka nchi zinazoendelea kuja China kushiriki kwenye mafunzo ya shahada ya pili ya "uongozi wa wanawake na maendeleo ya jamii".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako