• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Caster Semenya awasilisha rufaa nyingine katika mahakama ya Uswis

    (GMT+08:00) 2019-05-31 09:21:23

    Bingwa wa mbizo za mita 800 raia wa Afrika Kusini, Caster Semenya amewasilisha rufaa nyingine katika mahakama kuu ya Uswis, akipinga kushindwa katika kesi ya kuamua kuhusu kiwango cha homoni mwilini mwake.

    Mahakama ya kimataifa ya michezo, CAS ilitupilia mbali rufaa ya Afrika Kusini iliyokuwa inapinga sheria mpya za shirikisho la riadha duniani IAAF, zinazotaka wakimbiaji wa kike wenye homoni zaidi zipunguzwEe.

    Taarifa iliyotolewa Jumatano ya wiki hii inasema kuwa Semenya ataiomba mahakama ya Uswis itupilie mbali uamuzi wa Cas na kuongeza kuwa kiini cha rufaa yake ni haki ya msingi ya binadamu.

    Kwa sheria za sasa, Casater Semenya na wanariadha wengine wa kike ambao homoni zao zimezidi kiwango, watahitajika kutumia dawa maalumu ili kuzipunguza waweze kushindana katika mbio za kuanzia mita 400.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako