• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Joshua ajifua jijini New York akijiandaa kumvaa Ruiz

    (GMT+08:00) 2019-05-31 09:22:50

    Bingwa wa ngumi uzito wa juu duniani, Anthony Joshua amefanya mazoezi ya wazi mjini New York kuelekea pambano lake hapo kesho Juni 1 na Andy Ruiz mjini humo siku ambayo pia mabondia wa kike Delfine Persoon na Katie Taylor watapigana.

    Joshua mwenye urefu wa futi sita kwa sasa anashikilia mataji matatu kati ya manne; IBF, WBA na WBO akiwa na rekodi ya kushinda mapambano yake yote 22, kati ya 21 kwa knockout.

    Ruiz mwenye urefu wa futi nne amepoteza pambano moja na kushinda 32, huku 21 akishinda kwa knockout pia.

    Delfine Persoon wa Ubelgiji ndiye bingwa wa taji la WBC uzito wa Light na Katie Taylor wa Ireland anashikilia mataji ya WBA, IBF na WBO uzito huo wa Light

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako