• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yaongeza ushuru kwa Mexico ili kuiwekea shinikizo kuhusu suala la wahamiaji haramu

  (GMT+08:00) 2019-05-31 20:19:34

  Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kuwa Marekani itaongeza ushuru kwa asilimia 5 kwa bidhaa zote zinazonunuliwa kutoka Mexico kuanzia tarehe 10 mwezi Juni, ili kuilazimisha nchi hiyo kukabiliana suala la wahamiaji haramu wanaoingia nchini Marekani kupitia mpaka kati ya nchi hizo mbili. Serikali ya Mexico siku hiyo ilijibu kuwa, kama Marekani itatekeleza hatua ya kuongeza ushuru, Mexico itajibu vikali.

  Taarifa imesema kama Mexico ikitatua suala la wahamiaji haramu kwa hatua mwafaka, Marekani itafikiria kusamehe ushuru unaoongezeka. Lakini suala hilo likiendelea, ushuru utaongeza hadi asilimia 10 kuanzia tarehe 1 mwezi Julai, na kuendelea kuongeza hadi asilimia 25 katika miezi ijayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako