• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatumai Marekani kutambua hali halisi na kurudi kwenye njia sahihi

    (GMT+08:00) 2019-05-31 20:24:12

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesema vitendo vya upande mmoja na kujilinda kibiashara vya Marekani vinapingwa na watu wake, pia inalaumiwa na jumuiya ya kimataifa. China inatumai Marekani itatambua hali halisi, na kurudi kwenye njia sahihi haraka iwezekanavyo.

    Habari zinasema kuwa rais wa Marekani Donald Trump jana alisema Marekani imeshughulikia vizuri suala la biashara kati yake na China, na China inatamani sana kufikia makubaliano na Marekani. Amesema pande mbili ziliwahi kufikia makubaliano, lakini China iliyavunja. Pia amesema hatua za kuongeza ushuru kwa bidhaa za China zimeleta athari kubwa kwa China, zimesababisha viwanda vya utengenezaji nchini China kuhamia Vietnam na nchi nyingine za Asia, na China imekuwa dhaifu.

    Bw. Geng Shuang amesema, uongo kama huo wa Marekani sio wa mara ya kwanza, China inaonya Marekani isiamini uwezo huo wa kuzusha uvumi, na kupuuza uwezo wa wengine wa kutambua ukweli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako