• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atuma salamu za pongezi kwa mkutano wa 14 wa wakuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu

    (GMT+08:00) 2019-06-01 18:02:59

    Rais Xi Jinping wa China jana alituma salamu za pongezi kwa kufanyika kwa mkutano wa 14 wa wakuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu mjini Maka.

    Kwenye salamu zake, rais Xi amelipongeza shirika hilo kuwa ishara ya mshikamano wa nchi za Kiislamu na kutoa mchango muhimu katika kuhimiza ushirikiano kati ya nchi za Kiislamu katika miaka 50 iliyopita toka kuanzishwa kwake.

    Amesisitiza kuwa China ina uhusiano wa kirafiki na wa muda mrefu na nchi za Kiislamu, na pande zote mbili zinaungana mkono na kushirikiana kwa moyo wa dhati siku zote. Mbali na hapo amesema China inatilia maanani uhusiano huo wa kirafiki na nchi za Kiislamu, na kulichukulia Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu kuwa ni daraja muhimu la kufanya ushirikiano kati ya China na nchi za Kiislamu. Pia amesema China inapenda kushirikiana na nchi za Kiislamu katika kuinua uaminifu wa kisiasa, kuhimiza ushirikiano wa kiutendaji na mazungumzo kuhusu ustaarabu, na kutoa mchango katika juhudi za kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako