• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaeleza msimamo kuhusu mazungumzo ya kibiashara kati yake na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-06-02 10:36:19

    Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China leo tarehe 2 imetoa waraka ukieleza msimamo wa China kuhusu mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani. Hii ni mara nyingine kwa China kutoa waraka juu ya suala la mvutano wa kibiashara kati yake na Marekani, baada ya kutoa waraka unaoeleza ukweli wa mgogoro wa kibiashara kati ya pande hizo mbili mwezi Septemba mwaka jana. Mbali sehemu za utangulizi na mwisho, waraka huu wenye maneno 8,300 pia una sehemu tatu za katikati, ambazo ni pamoja na jinsi mgogoro huo uliozushwa na Marekani unavyoathiri maslahi ya nchi hizo mbili na ya dunia nzima, Marekani kuwa kigeugeu na kutokuwa na udhati kwenye mazungumzo ya kibiashara na China; China siku zote inashikilia kanuni za usawa, kunufaishana na uaminifu kwenye mazungumzo.

    Waraka huo unasema uhusiano wa kibiashara kati ya China na Marekani ni kama nguzo muhimu na chombo cha kusukuma mbele uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na unahusu maslahi ya kimsingi ya wananchi wa nchi hizo mbili, na ustawi na utulivu wa dunia.

    Waraka huo umeeleza kuwa tangu serikali mpya ya Marekani iingie madarakani mwaka 2017, imekuwa inatoa tishio kama kuongeza ushuru wa bidhaa na kuzusha migogoro wa kibiashara na wenzi wake wakuu wa kibiashara. Tangu mwezi Machi mwaka 2018, serikali ya Marekani imezusha mgogoro wa kibiashara na China, na China imelazimika kuchukua hatua za kukabiliana nao na kulinda kithabiti maslahi ya nchi na wananchi. Wakati huohuo, China siku zote inashikilia msimamo wake wa kutatua mgogoro kwa njia ya mazungumzo, na imefanya raundi nyingi za mazungumzo na Marekani kwa lengo la kutuliza uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

    Waraka huo umesema Marekani hivi karibuni ilitangaza kuongeza ushuru wa forodha wa bidhaa za China zinazoingia nchini Marekani, hatua ambayo haisaidii kutatua suala la kibiashara kati ya nchi hizo mbili, China inapinga vikali na inalazimika kujibu, ili kulinda maslahi yake halali.

    Waraka huo umesisitiza kuwa msimamo wa China ni endelevu na wazi, na kwamba China na Marekani zikishirikiana zitanufaika kwa pamoja, na zikipambana zitaumia kwa pamoja, na ushirikiano ni chaguo pekee sahihi kwa pande hizo mbili. China inapenda kuutatua mgogoro huo kwa njia ya ushirikiano, ili kuhimiza kufikiwa kwa makubaliano ya kusadiana na kunufaishana. Hata hivyo ushirikiano una msingi, na mazungumzo yana mstari wa mwisho, na kamwe China haitarudi nyuma katika masuala makuu ya kimsingi. China haipendi, haiogopi na inalazimika kushiriki wakati wa lazima katika vita ya kibiashara, msimamo huu ambao haujawahi kubadilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako