• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubabe wa kibiashara wa Marekani unaiathiri dunia

    (GMT+08:00) 2019-06-02 11:04:11

    China imesema mlolongo wa hatua zinazochuliwa na Marekani za kujilinda kibiashara zimevunja kanuni za Shirika la biashara duniani (WTO), kwa kuharibu mfumo wa biashara za pande zote, kuvuruga mnyororo wa uzalishaji na bidhaa duniani, na kutoa pigo kwa imani ya soko. Hatua hizo zimekuwa changamoto kali kwa juhudi za kufufua uchumi duniani, na tishio kubwa kwa mafungamano ya kiuchumi duniani.

    Hayo yamo kwenye Waraka kuhusu msimamo wa China katika mazungumzo kati ya China na Marekani, ulitolewa leo na serikali ya China. Waraka huo unasema hatua mpya za Marekani za kuongeza kiwango cha ushuru wa forodha dhidi ya China, na kuwekea vikwazo kampuni kadhaa dhidi ya China ikiwemo Huawei, zimedhuru maslahi ya pande mbalimbali, na China inazipinga kithabiti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako