• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafungua uchunguzi dhidi kampuni ya FedEx ili kulinda haki za wateja

    (GMT+08:00) 2019-06-02 11:06:24

    China imefungua uchunguzi dhidi ya kampuni ya FedEx ya Marekani kwa kusafirisha vifurushi kwa makosa. Taarifa rasmi iliyotolewa Juni Mosi na serikali ya China, inasema matukio kama hayo yanakiuka vibaya haki za kisheria na maslahi ya wateja wa kampuni inayosafirisha vifurushi, na pia yanakiuka vibaya sheria na kanuni za China.

    Kutolewa kwa taarifa hiyo kulitarajiwa na wengi, hasa baada ya tarehe 24 Mwezi uliopita kampuni ya FedEx iliposafirisha vifurushi viwili vilivyotakiwa kuja China kutoka kwenye ofisi za kampuni ya Huawei nchini Japan kuja China, kupelekwa Marekani. Kampuni hiyo pia ilijaribu kubadilisha safari ya vifurushi kutoka Vietnam vilivyotakiwa kwenda kwenye ofisi moja ya Huawei barani Asia, na kuelekezwa nchini Marekani.

    Licha ya kuwa kampuni ya FedEx imeomba radhi, imeendelea kusema matukio hayo yalikuwa ni makosa ya bahati mbaya ya ndani ya kampuni hiyo, na hayakutokana na ombi kutoka nje.

    Lakini, kutokana na kampuni ya Huawei kuongezwa kwenye orodha iliyotangazwa na Marekani ya makampuni ambayo usafirishaji wake wa bidhaa nje unadhibitiwa, ni kweli kosa hilo linaweza kuwa bahati mbaya? Ni vigumu kuamini hasa baada Bw. Edward Snowden kutoa ushahidi ukithtibitisha kuwa serikali ya Marekani ina uwezo wa kuingilia usafirishaji wa vifurushi. Kwa hiyo bila kujali kama matukio haya ni bahati mbaya za kiutendaji, au ni hatua za ushirikiano za "mkono mrefu wa mamlaka" wa Marekani, ni lazima dunia ifahamishwe.

    Kutokana na sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya huduma ya kusafirisha vifurushi ya China, makampuni yanayosafirisha vifurushi yanatakiwa kumlinda mtumaji, kwa maana ya kutotuma, kuficha au kufungua kifurushi cha mteja bila idhini yake, na makampuni hayo hayawezi kupeleka vifurushi hivyo kwa wengine. Baada ya idara husika za China kufanya mazungumzo ya makini na kampuni ya FedEx, sasa imefikia uamuzi wa kufungua shauri la kisheria ili uchunguzi kuhusu jambo hilo ufanyike. FedEx ikiwa ni kampuni ambayo imekuwepo nchini China kwa miongo kadhaa sasa, ina wajibu wa kushirikiana na mamlaka za China, ambazo zina haki ya kuiadhibu kulingana na matokeo ya uchunguzi yatakavyokuwa.

    China pia imeanzisha "orodha ya makampuni" yanayochukuliwa kuwa hayaaminiki, na itachukua hatua zinazohitajika za kisheria dhidi ya makampuni yatakayokuwa kwenye orodha hiyo. Uchunguzi dhidi ya kampuni ya FedEx utaweka mfano kwa makampuni na watu wasiofuata kanuni na sheria za China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako