• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ina udhati wa kufanya mazungumzo na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-06-02 11:44:21

    China imesisitiza kuwa uaminifu ni msingi wa mazungumzo, na kuisihi Marekani kuenenda kama nchi inayoaminika.

    Katika waraka kuhusu msimamo wa China katika mazungumzo ya kibiashara kati yake na Marekani uliotolewa leo na serikali ya China, China inasema siku zote inafanya mazungumzo na serikali ya Marekani kwa udhati na uaminifu. China inazingatia masuala yanayofuatiliwa na Marekani, ikijitahidi kutafuta njia na mbinu zinazoweza kuondoa tofauti za pande mbili. Mazungumzo yaliyofanyika kwa duru 11 yamepata maendeleo makubwa, yanalingana na maslahi ya China na Marekani, na ni matunda ya juhudi za pamoja. Katika mazungumzo hayo, China inazingatia uaminifu na ahadi. China imesisitiza mara kwa mara kwamba, pande mbili zikifikia makubaliano, China itatekeleza kwa makini ahadi ilizotoa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako