• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shinikizo la juu la Marekani lasababisha China na Marekani kushindwa kutatua tofauti zao zilizobaki

    (GMT+08:00) 2019-06-02 11:46:44

    Waraka uliotolewa leo kuhusu msimamo wa China katika mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani umesema, baada ya China na Marekani kuafikiana juu ya maudhui mengi ya makubaliano ya kibiashara, serikali ya Marekani haijatosheka na kutumia sera ya ubabe na mbinu ya shinikizo la juu, kutoa madai yasiyo na msingi, kukataa kufuta ushuru wa forodha ulioongezwa baada ya kuibuka kwa mgogoro wa kibiashara, na kulazimisha maudhui yanayohusu mamlaka ya China yaandikwe katika makubaliano. Hayo yote yamesababisha pande hizo mbili zishindwe kutatua tofauti zao zilizobaki.

    Waraka huo umesema hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru wa forodha mwezi Mei inakwenda kinyume na maoni ya pamoja yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili ya kutatua mgogoro kwa njia ya mazungumzo, inakwenda kinyume na matarajio ya watu wa nchi hizo mbili na wa nchi mbalimbali duniani, na kugubika mazungumzo ya kibiashara kati ya pande hizo mbili na ukuaji wa uchumi wa dunia. Waraka huo pia umesema China inalazimika kujibu kwa kuongeza ushuru wa forodha ili kulinda maslahi yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako