• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema vita ya kibiashara haijafanya Marekani "iwe nzuri tena"

    (GMT+08:00) 2019-06-02 11:50:33

    Waraka uliotolewa leo kuhusu msimamo wa China katika mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani umesema hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru wa forodha sio tu haikuhimiza ukuaji wa uchumi wa Marekani, bali pia kumesababisha hasara kubwa.

    Hasara hiyo ni pamoja na kuongeza gharama za uzalishaji za kampuni za China, kuongeza bei za bidhaa katika soko la ndani la Marekani, kuathiri ukuaji wa uchumi wa Marekani na maisha ya watu na kukwamisha uuzaji bidhaa kwa China. Ripoti iliyotolewa na Shirikisho la Wafanyabiashara la Marekani imeonyesha kuwa, kama Marekani ikitoza ushuru wa forodha wa asilimia 25 kwa bidhaa za China zinazoingia Marekani, pato la taifa la Marekani litapungua kwa dola za kimarekani trilioni moja katika miaka kumi ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako