• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya aweka urahisi wa kufanya biashara ili kuongeza kasi ya ukuaji uchumi

    (GMT+08:00) 2019-06-02 17:42:41

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta jana alitoa maelekezo mawili ya sera ili kuondoa vikwazo vinavyosababisha kupungua matumizi ya jumla na shughuli za biashara kwenye uchumi.

    Akihutubia kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 56 ya siku ya Madaraka huko Narok, kusini magharibi mwa Nairobi, rais Kenyatta amewaelekeza wahasibu wa serikali kushughulikia malipo yote yanayosubiri ambayo hayana hoja za ukaguzi kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa fedha, Juni 30. Pia ameilekeza Hazina ya Taifa kuhakikisha inafuata kwa ukamilifu maelekezo ya kushughulikia malipo yanayosubiri na kuzitaka serikali za kaunti kufuata utekelezaji huo.

    Amesisitiza kuwa malipo yote ya vifaa yaliyotolewa kwa ajili ya taifa na serikali za kaunti lazima yashughulikiwe haraka na kupewa kipaumbele, akisema maelekezo yanaendana na sera ya serikali ya kuhimiza viwanda na makampuni ya ndani, ya "Nunua Kenya Jenga Kenya."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako