• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yahimiza mpango wa usalama wa mpito nchini Sudan Kusini kuelekea utekelezaji wa makubaliano mapya ya amani

    (GMT+08:00) 2019-06-03 09:06:23

    Shirika la Maendeleo ya Kiserikali la nchi za Afrika Mashariki (IGAD) limezihimiza pande zote za Sudan Kusini kujiunga kihalisi na mpango wa usalama katika muda wa mpito na kutekeleza makubaliano mapya ya amani kwa wakati.

    Taarifa iliyotolewa na Mjumbe maalum wa Shirika hilo nchini Sudan Kusini Bw. Ismael Wais imesema, utekelezaji wa makubaliano ya kumaliza mgogoro nchini Sudan Kusini kwa kiasi kikubwa unahusiana na mipango ya usalama katika muda wa mpito.

    Makubaliano mapya ya amani ya Sudan Kusini yanataka pande zote zinazopambana ziungane tena, lakini mchakato huo umeshindwa kukamilika kutokana na baadhi ya makundi kukataa kutangaza ukubwa wa makundi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako