• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuidhinisha leseni za teknolojia ya 5G kwa matumizi ya kibiashara

    (GMT+08:00) 2019-06-03 19:23:01

    Wizara ya viwanda na teknolojia ya habari ya China MIIT leo imesema itaidhinisha leseni za teknolojia ya 5G kwa matumizi ya kibiashara hivi karibuni.

    Wizara hiyo imesema sekta ya teknolojia ya 5G ya China ina uwezo mkubwa wa ushindani kupitia uvumbuzi wa ndani na ushirikiano wa ufunguaji mlango. Imeongeza kuwa kiwango cha teknolojia ya 5G ni cha kimataifa na kimewekwa kwa pamoja na mashirika husika duniani kote. Hivi sasa China inachukua zaidi ya asilimia 30 ya vibali vikuu muhimu kwa teknolojia hiyo.

    Makampuni mengi ya nchi za nje ikiwa ni pamoja na Nokia, Ericsson, Qualcomm na Intel yameshiriki kwenye majaribio hayo, na teknolojia ya 5G ya China iko tayari kwa ajili ya matumizi ya kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako