• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi asisitiza umuhimu wa kutenganisha taka

    (GMT+08:00) 2019-06-03 19:24:00

    Rais Xi Jinping wa China amesisitiza juhudi za kulea desturi ya kutenganisha taka, ili kuboresha mazingira ya kuishi na kuchangia maendeleo endelevu na yasiyo na uchafuzi.

    Rais Xi amesema kutenganisha taka kunahusiana na usafi wa mazingira ya watu na matumizi ya raslimali kwa kubana matumizi. Pia amesema desturi hiyo ni muhimu kwenye kiwango cha kuelewa mambo ya uraia.

    Rais Xi pia amesema kupitia usimamizi na mwongozo, China inaweza kufanya watu washiriki zaidi kwenye kuendeleza desturi ya kutenganisha taka, kuboresha mazingira ya kuishi na kuchangia maendeleo endelevu yasiyo na uchafuzi.

    Mwezi Desemba mwaka 2016 Rais Xi aliendesha mkutano wa kundi linalosimamia mambo ya fedha na uchumi, lililokuwa linafanya utafiti kuhusu kutenganisha taka, na yeye mwenyewe alifanya ziara kujionea utenganishaji wa taka katika ngazi ya jumuiya, ili kutoa maelekezo kwa ajili ya kazi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako