• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NDONDI: Deontay Wilder afurahia kipigo cha Joshua asema alikuwa akishinda kwa kubebwa.

    (GMT+08:00) 2019-06-04 07:55:04
    Bondia wa uzani wa juu kutoka nchini Marekani Deontay Wilder ameshindwa kuficha hisia zake juu ya pambano ndondi ambapo bondia Anthony Joshua alinyukwa na Andy Ruiz Jr.

    Wilder mara kadhaa amekuwa akimtuhumu Joshua kwa kuzuia pambano lao kwa kutengeneza vikwazo lukuki ili wasikutane ulingoni.

    Amesema, Joshua amekuwa akishinda mataji kwa kubebwa lakini safari hii amekutana na kisiki na ndio maana amepigwa. Promota wa Joshua Eddie Hearn ametangaza kuwa bondia wake atarejeana na Ruiz kabla ya mwaka kuisha kwenye mwezi Novemba ama Disemba jijini London.

    Hearn amebainisha kwa kwa sasa mazungumzo yoyote ya kuzipiga dhidi ya Fury ama hata Wilder yamesitishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako