• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kunadi maeneo ya uwindaji kwenye mtandao

    (GMT+08:00) 2019-06-04 09:04:35

    Naibu kamishna wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania TAWA Bw. Imani Nkuwi amesema Tanzania itapiga mnada maeneo yake ya uwindaji kupitia mtandao wa internet kuanzia Juni 10, hatua inayolenga kuimarisha uwazi na kuzuia ufisadi kwenye sekta ya utalii.

    Bw. Nkuwi amesema TAWA inatoa mafunzo maalumu kwa waendeshaji wa huduma za kitalii na kampuni za safari za uwindaji kuhusu namna ya kuingia kwenye tovuti ya Wizara ya Maliasili na Utalii na kutoa zabuni kwenye mnada huo. Ameongeza kuwa kwa njia hiyo, thamani ya maeneo ya uwindaji itaamuliwa na soko.

    Kwa mujibu wa ofisa huyo, kipindi cha kwanza cha mnada huo kinatarajiwa kuanza Juni 10 hadi 17, ambapo Jumla ya maeneo 26 ya uwindaji yatanadiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako