• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ICRC yasaidia kuwarudisha makwao watu 17 walioshikiliwa nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2019-06-04 09:08:06

    Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ICRC imesema imetoa msaada wa kuwarudisha makwao wafuasi 17 wa makundi yenye silaha ya Somaliland na Puntland ambao walitekwa wakati wa mapambano ya kisilaha yaliyoibuka mwezi Mei mwaka jana.

    Mkurugenzi wa Ujumbe wa ICRC nchini Somalia Bw. Simon Brooks amesema, shirika hilo limewarudisha watu hao walioachiwa huru kwenye eneo la Hargeisa la Somaliland na Garowe la Puntland. Pia amesema, shirika la msalaba mwekundu limetoa huduma kwa pande mbili hasimu na kuthibitisha utayari wake wa kutoa msaada chini ya maombi ya pande hizo, kuwarudisha makwao watu wote 17 waliotekwa.

    Mapambano ya kisilaha kati ya Somaliland na Puntland yalitokea mwezi Mei mwaka jana kwenye eneo la Tukaraq, na kusababisha vifo na majeruhi na wengine wengi kukimbia makazi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako