• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu watoa mwito kwa watafiti wa Afrika kupata utatuzi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2019-06-04 09:13:19

    Wataalamu wa Kenya jana wametoa mwito kwa watafiti wa hali ya hewa wa Afrika kupata utatuzi wa kupunguza hatari zinazokabili bara hilo kutokana na mabadiliko ya tabianchi na majanga yanayosababishwa na mabadiliko hayo.

    Mhadhiri wa masuala ya hali ya hewa wa chuo kikuu cha Nairobi, Laban Ogallo amesema, inahitaji kukuza uchunguzi kuhusu hali ya hewa na kuimarisha uwezo wa kushirikisha wadau wengine. Amesema tofauti ya ujuzi kuhusu hali ya hewa inatokana na ushirikiano dhaifu wa uchunguzi wa pamoja ambao umesababisha utafiti usio wa kutosha kuhusu matukio mabaya ya hali ya hewa na athari zao.

    Ogallo amewataka wanasayansi vijana washiriki kwenye utafiti ambao utasaidia utekelezaji wa ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika, malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa na makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako