• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika yakabiliwa na changamoto nyingi katika kukinga na kutibu ugonjwa wa UKIMWI

    (GMT+08:00) 2019-06-04 09:24:50

    Balozi wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Lazarus Amayo jana amesema, Afrika bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika kukinga na kutibu ugonjwa wa UKIMWI.

    Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI, balozi Amayo amesema, elimu ya kujikinga na ugonjwa huo kwa vijana wengi katika miaka 20 iliyopita haijaendelezwa, na kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo kati ya wasichana na wanawake vijana ni cha juu sana.

    Balozi Amayo amesema, kwenye eneo la Afrika magharibi na kati, upungufu wa fedha, mifumo dhaifu ya afya, malipo rasmi na yasiyo rasmi kwa hudumu za afya, hali ya kibinadamu na ubaguzi vimeharibu juhudi za upimaji na matibabu ya ugonjwa wa UKIMWI.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako