• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eneo la kusini mwa Afrika laripoti kiasi cha chini zaidi cha mvua wakati wa msimu wa kilimo kuanzia 1981

    (GMT+08:00) 2019-06-04 09:35:03

    Kiasi cha mvua katika eneo la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa msimu wa kilimo kuanzia Oktoba mwaka 2018 hadi mwezi Machi mwaka 2019 kilikuwa cha chini zaidi katika miaka 38 iliyopita.

    Taarifa iliyotolewa katika mkutano wa mawaziri wa Jumuiya hiyo wanaoshughulikia kilimo, usalama wa chakula, uvuvi na ufugaji wa samaki imesema, uhaba wa mvua pia umeathiri maeneo ya malisho ya mifugo na mifugo, na pia upatikanaji wa maji kwa matumizi ya binadamu na kilimo.

    Pia nchi tatu za SADC zimetangaza janga la ukame kutokana na uhaba wa mvua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako