• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Zimbabwe laanza kujadili muswada wa sheria ya uwekezaji

    (GMT+08:00) 2019-06-04 09:46:01

    Kamati mbili za muundo wa uwekezaji za bunge la Zimbabwe zimeanza majadiliano ya wazi juu ya mswada wa sheria ya idara ya uwekezaji na maendeleo, ambayo inalenga kurahisisha biashara nchini humo kwa kuanzisha kituo kinachoshughulikia mambo yote ya uwekezaji.

    Muswada huo pia unataka kuanzisha idara itakayochukua majukumu ambayo sasa yanatekelezwa na Mamlaka ya Uwekezaji, Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Kiuchumi, na Kitengo cha Ubia cha wizara ya fedha na maendeleo ya uchumi.

    Muswada huo unataka serikali kuwatendea wawekezaji wa kigeni kwa usawa, na kuhakikisha kuwa mali zao hazichukuliwi, na endapo zikichukuliwa kutokana na madhumuni ya umma, wawekezaji wa kigeni watalipwa fidia bila ya ubaguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako