• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi 53 za Afrika kushiriki katika maonesho ya kwanza ya biashara kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2019-06-04 18:40:22

    Nchi 53 za Afrika zimethibitisha kushiriki katika maonesho ya kwanza ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika yanayopangwa kufanyika kuanzia Juni 27 hadi 29 mkoani Hunan, katikati mwa China.

    Naibu mkuu wa mkoa huo Bw. He Baoxiang amesema, mashirika ya kimataifa likiwemo Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa, Shirika la Mpango wa Chakula la Dunia na Shirika la Biashara la Dunia pia yatatuma wajumbe kushiriki kwenye maonesho hayo.

    Pia amesema maonesho hayo yatakayofanyika mjini Changsha, mji mkuu wa mkoa huo yatahudhuriwa na wageni zaidi ya 1500 kutoka nje na wengine zaidi ya elfu 5 kutoka ndani, pamoja na wanaofanya maonesho, wateja na wageni maalumu zaidi ya 3500.

    Ameongeza kuwa mpaka sasa kumekuwa na miradi kadhaa ya ushirikiano, inayohusisha ushirikiano na nchi 39 za Afrika. Vilevile miradi ya uwekezaji na biashara itasainiwa katika maonesho hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako