• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • VOLIBOLI: Kenya yaanza vyema kwa kuwatwanga Uganda

    (GMT+08:00) 2019-06-05 08:20:58
    Wenyeji Kenya wamefaulu kulipiza kisasi dhidi ya Uganda baada ya kubwaga kwa seti 3-2 katika mechi yao ya ufunguzi ya michuano ya voliboli ya wanaume ya kufuzu kushiriki mashindano ya Afrika (African Games) katika ukumbi wa kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi.

    Katika mechi ya kufungua mchujo huu wa ukanda wa tano unaoshirikisha mataifa manne pekee, mabingwa mara tano wa voliboli ya African Games, Misri wamecharaza Rwanda kwa seti 3-1. Bingwa wa michuano hii atakata tiketi ya kushiriki makala ya 12 ya mashindano ya African Games yatafanyika nchini Morocco kutoka Agosti 19 hadi 31 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako